KATIKA kuendelea kujiweka fiti kwa ajili ya msimu ujao, klabu ya Yanga imemsajili beki wa kati wa Toto African, Ladislaus Mbogo Boniface maarufu kwa jina la Mnyama.

Usajili huyo umekuja ikiwa ni siku chache baada ya kumnasa Kelvin Yondani kutoka Simba, hali ambayo inaonyesha Yanga imejipanga vizuri kuimarisha ukuta wake baada ya kushika nafasi ya tatu msimu uliopita katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimeeleza kuwa uongozi umekubali kumsajili beki huyo lakini atafanyiwa operesheni ndogo kuondoa uvimbe uliopo shavuni.

“Ni kweli tumemsajili, ni beki mzuri wa kati na tuna imani atatusaidia msimu ujao, ila itabidi apatiwe matibabu ya uvimbe alionao shavuni,” kilisema chanzo CHETU.

SOURCE:globalpublishers