YAWEZEKANA majaaliwa ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kurejea Simba yakawa ni magumu kwa kuwa kitendo cha klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini kumpa nafasi ya kucheza katika mechi dhidi ya Newcastle United ni imani kuwa wamemkubali.
Okwi ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitakiwa na klabu za nchini humo ikiwemo Kaizer Chiefs amepewa nafasi ya kucheza katika mechi hiyo wakati Orlando ina wachezaji wengi na wenye vipaji ambao wanaweza wasipate bahati ya kucheza katika mechi hiyo.
Uongozi wa Simba tayari umethibitisha kupokea barua hiyo ya mwaliko wa Okwi ambapo kinachoendelea ni wao kutoa jibu la kumruhusu.