Habari za Hivi Punde kutoka Kijiji cha Kinyenze, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro zinadai kuwa Mashamba ya wananchi yaliyo na Minazi, Migomba, Miwa na Mazao mengine ya kudumu yaliyo porwa na Mwekezaji wa Kizungu kwa kuzungushiwa uzio yanateketea kwa Moto mkubwa. Chanzo cha Moto huo inasemekana ni Walizi wa Mzungu huyo ambao huingia shambani humo mara kwa mara na kuiba mazao mashambani humo ndio wamesababisha moto huo ambao utaleta hasara kubwa.

Hivi Karibuni Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Vijana , Amos Makala aliitisha Mkutano wa kutatua Mgogoro huo uliodumu kwa miaka miwili sasa lakini Mkurugenzi wa Mvomero aliahirisha Kikao hicho kwa madai ya kuambiwa na DC wa Mvomero hadi alijue tatizo hilo kwa undani ndipo ashiriki Mkutano na Wananchi.

Kuchomwa kwa mashamba hayo huenda kukaleta mzozo mkubwa baina ya wananchi na Mwekezaji huyo.

SOURCE: