Mwanaharakati wa demokrasi nchiniBurma, Aung San Suu Kyi, hatimae ametoa hotuba yake ya Nobel, miaka 21 baada ya kutunukiwa tuzo ya amani, ambayo hakuweza kuipokea rasmi wakati huo.
Alisema tuzo hiyo iliufungua moyo wake, na kumfanya ahisi kuwa yuko pamoja na ulimwengu ingawa alikuwa kifungoni.
Aung San Suu Kyi alisema tuzo hiyo pia ilihakikisha kuwa juhudi za kupigania demokrasi na haki za kibinaadamu nchini Burma na dunia nzima, zinaendelea na kufanikiwa.