Mwakilishi wa Tanzania katika Mashindano ya Miss World 2012, Lisa Jensen akipunga mkono baada ya kushinda nafasi hiyo katika shindano dogo lililofanyika jana jijini Dar es Salaam na kushirikisha warembo 10 waliowahi kushiriki fainali za Miss Tanzania miaka ya nyuma. Lisa aliwashinda warembo wengine 9.

Redd’s Miss World Tanzania, Lisa Jensen (katikati) akivishwa taji hilo na Miss Tanzania,Salha Israel katika hafla fupi iliyomalizika usiku huu kwenye kiota kipya cha maraha cha 327,Mikocheni jijini Dar es Salaam.kulia ni mshindi wa tatu kwenye kinyang’anyiro hicho,Pendo Laizer . Lisa amewashinda warembo wengine 9 katika shindano hilo dogo la kutafuta Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Mwaka huu ya Miss World.

Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya Tano Bora wakilamba picha ya pamoja

Washiriki wote kumi wakiwa katika picha ya pamoja na mavazi yao ya kutokea usiku