Afisa mkuu kwenye bunge la Misri, aliiambia BBC kwamba amepokea barua kutoka halmashauri ya kijeshi kumuarifu rasmi kuwa bunge limefutwa.
Siku ya Alkhamisi, Mahakama ya Katiba yaliamua kuwa uchaguzi wa bunge uliofanywa mwaka jana ulikwenda kinyume na katiba.
Tangazo hilo limetolewa wakati Wamisri wanapiga kura kumchagua rais mpya atayechukua nafasi ya Hosni Mubarak, ambaye alitolewa madarakani mwaka uliopiota