Polisi mpelelezi Yohana (kulia) akimpeleka mahakamani mtuhumiwa wa wizi wa shilingi 53,620,178 mali ya kampuni ya mafuta ya Camel ya mjini Singida, Bw. Jumapili Mussa.

Mtuhumiwa Jumapili akiwa ameketi katika chumba cha mahakama cha mkoa mjini Singida akisubiri kesi yake kutajwa.


Meneja wa kituo cha mafuta cha Camel Oil com ltd kilichopo Kibaoni Singida mjini, Jumapili Mussa (47)ameburuzwa mbele ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida akituhumiwa kutenda makosa mawili likiwemo la kumwibia mwajiri wake shilingi milioni 53.6.

Mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Maria Mdulugu alidai mbele ya hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Ruth Massamu kuwa kati ya januari nane na juni 30 mwaka huu katika muda usiofahamika mshitakiwa Jumapili alikula njama ya kuandaa nyaraka badia, kuhusiana na malipo ya zaidi ya shilingi milioni 53.6 kwa nia ya kumdanganya mwajiri wake.

Alisema mshitakiwa Jumapili alitenda kosa hilo huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Mshitakiwa Jumapili,amekana makosa hayo yote.

Mahakama hiyo,imempa mshitakiwa mashariti ya dhamana ikiwa ni kuwa na wadhamini watatu wenye mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 53.6.

Wakati mwandishi wa habari hizi akiondoka mahakamani hapo ndugu na jamaa wa mshitakiwa Jumapili, walikuwa wakiendelea na taratibu ya kumwekea dhamana.

Kwa kipinid hicho mshitakiwa Jumapili tayari alikuwa ameishapelekwa mahabusu ya gereza la wilaya ya Singida.

source:dewjiblog