Petr Jiracek alifunga bao la pekee katika mechi ya uwanja wa Wroclaw dhidi ya wenyeji Poland siku ya Jumamosi, na kuwahuzunisha mashabiki wa nyumbani, wakati Jamhuri ya Czech ilipofuzu kuingia robo fainali za mashindano ya Euro 2012.
Nae Giorgios Karagounis, nahodha wa timu ya Ugiriki, alifunga bao moja katika mtanange na Urusi, na hivyo kufanikiwa kuiondoa Urusi katika mashindano hayo kwa bao hilo moja