Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Wapili kutoka kushoto ni Kaimu Mkrugenzi wa Idara la Uendeshaji wa Shirika hilo kapteni Richard Saidi. Hafla hiyo ya utoaji vyeti kwa wahitimu ilifanyika katika Makao makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam wikiendi hii. Picha na mpiga picha wetu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi bora wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL katika hafla ya utoaji vyeti kwa wanafunzi 39 waliomaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi wa shirika hilo Patrick Itule na Kaimu Mkrugenzi wa Idara la Uendeshaji wa Shirika hilo kapteni Richard Saidi (Kulia). Picha na mpiga picha wetu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro akihutubia wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege katika hafla yakuwakabidhi vyeti iliyofankika Jijini Dar es Salaam jana

Tumeiva sasa. Wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL wakionyesha vyeti walivyokabidhiwa baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana. Picha na mpiga picha wetu.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL kilichopo Terminal 1 Lawrence Mhomwa akihutubia wahitimu wa chuo hicho katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimun hawa baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmoja wa waalimu wa Chuo hicho Thecla Ndussi.

Wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL waonyesha nyuso za furaha mbele ya kamera ya blogu hii katika hafla ya kukabidhiwa vyeti baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana


Wahitimu wa Chuo cha Mafunzo cha ATCL wakipozi kwa picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhiwa vyeti baada ya kumaliza kozi ya utoaji huduma kwenye ndege .Hafla hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam jana. Picha na mpiga picha wetu.

SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limetangaza mpango wakuungana na Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) ilikutoa mafunzo mbalimbali yatakayowezesha upatikanaji wa wataalam mbalimbali wa sekta ya anga.

Akizungumza katika sherehe yakuwaga wanafunzi 39 wa Chuo cha Mafunzo cha Shirika la Ndege la Air Tanzania jijini Dar es Salaam wikiendi hii, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Lusajo Lazaro alisema mpango huo ambao utakuwa endelevu umewekwa kwa makusudi ilikuhakikisha wataalam katika sekta ya usafiri wa anga wanakuwa na ubora unaostahili hususani wakati huu ambapo sekta ya usafiri wa anga inakuwa kwa kasi zaidi na kuvutia wawekezaji zaidi. “Tumeshasaini nyaraka za makubaliano (MOU)na NIT ilikuwezesha ufanisi wa swala hili. Nimatumaini yetu kuwa mpango huu utasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa wataalam katika sekta ya anga nchini.

”Bila pingamizi lolote kuwa sasa tutahitaji wataalam zaidi ili kuboresha utoaji wa huduma zetu hususani katika kipindi hiki ambacho tumejikita katika utekelezaji wa mpango wetu wa maendeleo wa miaka mitano ambao unalengo la kuongeza safari na ndege nyingine katika miaka michache ijayo,” alisema. Lazaro akitoa maoni yake juu ya soko la pamoja la Afrika Mashariki ambalo limefungua milango kwa biashara huria za bidhaa na huduma ndani ya nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) alisema kuwa kampuni yake imejipanga kutumia fursa hiyo ipasavyo.

“Soko hili huria la pamoja litatengeneza fursa nyingi sana na tayari sisi kama shirika tumejipanga kuchangamkia na kuzitumiua fursa hizo ipasavyo. Tupo katika mipango ya kuongeza safari zetu zaidi na pale inapowezekana kutafanyakazi pamoja na mashirika makubwa barani. Tunahitaji wafanyakazi wenye ujuzi na walio bora ambao watatusaidia kuleta ushindani kama shirika,” aliongeza.

Kwa upande wake, mhitimu wa Chuo cha Mafunzo cha Mafunzo ya Anga cha ATCL Yasmin Khanj akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake waliohitimu alisema kuwa watatumia vizuri ujuzi wote walioupata katika chuo hicho ilikuchangia maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga nchini.

“Hii ni hatua kubwa sana katika maisha yetu. Tunaiomba kampuni ya ATCL kutupa fursa ya kupata ujuzi zaidi kwa kutupatia nafasi kwenye kampuni ili tuweze kupata uzoefu unaohitajika ili tulete ushindani na kutoa huduma ipasavyo,” alisema.

Aidha, mkuu wa chuo cha mafunzo cha ATCL, Lawrence Mhomwa alisema kuwa wahitimu hao baada ya kumaliza mafunzo yao yaliyojumuisha mada saba katika chuo hicho zikiwa pamoja na huduma kwa wateja, usalama katika viwanja vya ndege, uhudumu ndani ya ndege, usalama ndani ya ndege na mada nyingine,wahitimu hao sasa wanauwezo wa kufanyakazi katika shirika lolote la ndege

source:fatherkidevu