MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, anatarajia kumdondosha nyota wa filamu wa Nigeria, Omotola Jalade hapa nchini.

Wema Sepetu, ambaye kwa sasa anatamba kwenye tasnia ya filamu anatarajia kumleta Omotola kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa filamu yake mpya iitwayo Super Star.

Filamu hiyo ya Super Star, inazungumzia maisha ya Wema kuanzia utotoni kushiriki kwake Miss Dar Indian Ocean, Miss Kinondoni, Miss Tanzania hadi kuingia kwenye filamu.

Kwenye filamu hiyo Wema ameshirikiana na wasanii mbalimbali akiwemo mwimbaji wa Machozi Band, aitwaye Mwinyi.

Omotola, ambaye atatua Tanzania wiki hii, alianza kutamba kwenye tasnia hiyo baada ya kutoka na filamu iitwayo Iva mwaka 1993.

Hadi sasa nyota huyo amecheza jumla ya filamu 52, zikiwemo, Ties That Bind (2011), A Private Storm
Ije (2010), My Last Ambition (2009), Beyonce & Rihanna (2008), Temple of Justice (2008), Tomorrow Must Wait (2008) na nyingine nyingi.