Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba juma hili anatarajia kuidhinishwa kujiunga na klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34 raia wa Ivory Coast inasemekana amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu wenye thamani ya paundi milioni 25.
na haya ni maneno yake kwenye page yake ya facebook “Today I can inform you that I have signed with Chinese club Shanghai Shenhua FC for a two and a half year deal”