Malkia Khadija Kopa

May 22 mwaka huu mwimbaji staa wa Taarab Khadija Kopa alitoa taarifa kwenye kipindi AMPLIFAYA kuwa gari lake aina ya Noah lililokua limelazwa sehemu ya kulaza magari kwa kulipia Mwananyamala Dar es salaam kuwa limeibiwa .

Wezi waliohusika hawakuliwasha wakati wa kuiba, waliliburuza hadi mbali kidogo ndio wakaliwasha hilo na magari mengine mawili likiwemo la msanii wa bongo fleva Dogo Hamidu ambae alilipata lake maeneo ya Mlimani City Dars es salaam zaidi ya wiki moja baadae.

Alichoniambia Khadija Kopa jana usiku ni kwamba gari lake limepatikana jana mchana, limekutwa moshi lilikua limeuzwa kwa mtu ambae nae baadae aliliweka rehani kwa mtu mwingine tu likawa limehifadhiwa.

Mpaka limepatikana tayari limetolewa rim zote na zimeuzwa kwa mtu mwingine, Jambazi anaedaiwa kuhusika na wizi wa magari yote kwa mujibu wa Khadija Kopa anaitwa Rinko alikamatwa juzi na magari yote yaliyoibwa matatu yalikua chini yake.

Kwenye sentensi nyingine Khadija kopa amekanusha stori zilizotangazwa mwanzoni mwa wiki iliyopita kwamba amemtungia wimbo mwizi huyo wa gari lake.