Logo hii imekuwa kitambulisho kikubwa kwa kuutangaza muziki wa bongo flava duniani kote. Logo hii imesambaa kila kona ya dunia kwa kupitia mitandao ya kijamii. Je unamjua aliyetengeneza logo hii?? Na ni lini aliitengeza logo hii?? Na sasa itumika kwenye mitandao gani duniani?.
Logo hii ina tumika Kama kitambulisho cha muziki wa Bongo Flava, ambao asili yake ni hapa nchini Tanzania na pia logo hii imetengenezwa humu humu Nchini Tanzania.Logo hii ilivumbuliwa na kutengenezwa na Michael Mlingwa, ambaye anajulikana sana kama MxCarter. Na pia anatumia jina hilo la “MxCarter” kama username yake kwenye mitandao yote yakijamii. Michael alitengeza Logo hii alipokuwa anatangaza kazi za wasani wa BongoFlava kwenye mitandao ya kijamii, Ambapo alikuwa Editor na Mmoja ya waazilishi wa blog ya “BABKUBWA” ambayo ilikuwa maarufu sana miaka ya nyuma kidogo ambapo Mike alikutana na Mwazilishi mwenzie wa Blog Hiyo Bwana Ralph Godden. Ambapo Ralph alimkuta Michael tayari anaupeo na malengo ya kunyanyua muziki wa Bongo Flava ndipo wakaamua kutengeneza Blog hiyo.

Michael “MxCarter” Mlingwa.

Michael Milingwa alitengeneza Logo hii ya Bongo Flava Swahili Hip hop Mei 2009. Wakati akiwa Babkubwa anatangaza muziki wa kitanzania mtandaoni, na alitumia logo hii kutengeneza Facebook Fan Pages za wasani mbalimbali maarufu nchini Tanzania. Mpaka sasa Logo hii inazunguka katika mitandao mingi duniani pamoja na blog nyingi zilizopo nchini Tanzania. Ambapo sasa logo hii imekuwa “official ICON” ya Muziki wetu wa bongoFlava.
Mpaka sasa Michael anaendelea kutangaza na kukuza Muziki waKitanzania zaidi na zaidi, na anamilikia blog yake kubwa inayoitwa “GongaMx’’ na amakekuwa mshauri mkubwa sana kwa wasani wa kitanzania kwenye swala lakutangaza kazi zao mitandaoni, na kuwa saidia wasani hao kuwa na website , na blog zao amabazo zina tambulisha kazi zao. Michael nikijana ambaye anakipaji kikubwa mno , kwa lugha za kigeni tutaita “Multitalented guy”. Na Mtu anayependa kuona wengine wanafanikiwa katika Maisha yake na kazi zake. Kwa watu wanaye mjua Michael hawatanikatalia kuhusu sifa za Michael Mlingwa.
Logo hii sasa inatumika kwenye mitandao mikubwa ya kijami kama Facebook, youtube, soundclouds,myspaces, reverbnation, twitter, kwenye blog nyingi za Tanzania, kwenye google, yahoo na bing. N.k
Unaweza kuwasiliana nae kwa kupitia mtandao wa twitter by following @MxCarter