Kanye West amezipalia moto fununu kuwa anataka kuuliza lile swali tamu katika masikio ya wasichana wengi (will you marry me?) kwa mpenzi wake Kim Kardashian,kwa kudaiwa kuitengeneza mwenyewe pete ya uchumba kwaajili ya kumvisha nyota huyo wa reality TV shows!
Rapper na produsa huyo anaonekana kutaka kuupeleka uhusiano wao hadi hatua nyingine kubwa na inasemekana kwamba ameomba msaada kwa shemeji zake Khloe na Kourtney katika kudesign pete mahsusi ya kumvisha Kim.
Kim mwenye miaka 31 na ambaye yupo kwenye mchakato wa kupewa taraka na aliyekuwa mume wake mchezaji wa NBA Kris Humphries, anaonesha kuwa bado hajakata tamaa ya kuolewa tena, na anadai kuwa Kanye ndo mpango mzima!
Chanzo kimoja kimeliambia jarida la Uingereza la Closer,
“Alipoolewa na Kris, alijua ndani kabisa kuwa haikuwa sawa, lakini anasema anajua anataka kuishi maisha yake yote na Kanye na anadhani Kanye anafikiria hivyo pia. Anataka watoto mapema hivyo ndoa ni hatua asili.”
“Kanye alimuomba mama yake Kim (Kris) ampe ushauri wa pete, lakini alimwambia awaulize shemeji zake Khloé na Kourtney, kwakuwa Kim aliwaambia dada zake kuwa anataka kitu tofauti kabisa kwa pete yake ya mwisho. Kanye ana sonara mjini New York ambaye wamekuwa wakijadiliana mawazo,” kiliongeza chanzo hicho.
Kim ameweka wazi kuwa awamu hii anataka harusi ya kawaida tu ukilinganisha na harusi yake ya kifahari na Humphries iliyogharimu dola milioni kumi. Chanzo hicho kimeendelea,
“Yeye na Kanye wamesema, kama wakioana, wangependa kuwa na harusi ndogo ufukweli huko L.A. Ni kama vile Kim amebaini kuwa ni mwanaume na sio harusi ya nguvu inayotengeneza ndoa.
“Anahofia kile watu watafikiria, lakini marafiki na familia yake wamemwambia afanye kile kinachompa furaha.
“Wanasubiria taraka (ya Kris Humphries), kisha watavishana pete.”