Mchungaji wa nchini Uganda William Muwanguzi a.k.a Pastor Kiwedde amerejeshwa rumande kwa tuhuma za kula njama na wenzie waliombaka mwanamke wa miaka 30.
Makamu mzungumzaji wa polisi, Judith Nabakooba amesema Kiwedde na wanaume wenzie watatu, wakisafiri katika gari binafsi waliwachukua wanawake wawili kutoka pub ya Kabuusu na kuwapa ofa ya kwenda kunywa.
Wanawake hao baadae walipatwa na wasiwasi na kujaribu kutoroka ambapo mmoja wao alifanikiwa, wakati aliebaki alibakwa na wanaume hao wawili.