Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 46 huko India amesema hajutii kumuua kwa kumkata kichwa mwanae wa kike mwenye umri wa miaka 20 kutokana na mtoto huyo kuwa na uhusianoa wa kimapenz na wanaume ambao baba yake alikua hawataki.

Mwanaume huyo aitwae Oghad Singh amejisalimisha polisi akiwa ameshika kichwa cha mwanae na panga alilotumia kukikata huku raia wa kijiji anachotoka wakishangaa.

Mwanaume huyo amesema alifanya hicho kitendo pia kutokana na mwanae kuidhalilisha familia na huenda ingepelekea dada zake wakakosa waume ambapo kama ilivyo desturi na mila za wahindi mama mzazi na dada wanne wa marehemu hawakuruhusiwa kuhudhuria mazishi yaliyotawaliwa na vilio na mshangao mkubwa.

Shirika la habari la AP limeripoti kwamba Kitendo hicho cha kinyama alichokifanya huyo baba huyo ni nadra sana kutokea kwenye nchi hiyo yenye watu zaidi ya bilioni 1.2.

Kama unapenda na watu wako waisome hii habari unaweza kulike hapo chini sehemu ya facebook au kutweet, naomba radhi kwa kuchelewa kuiweka kama nilivyoahidi mtu wangu wa nguvu.

infosource:Ayo