Luis Figo

Hivyo Ureno anamsubiri mshindi atakayepatikana kati ya Hispania na Ufaransa. Robo fainali ya kwanza katika mashindano ya kandanda ya kuwania taji la ubingwa wa mataifa ya ulaya, Euro 2012 imekamilika kwa Ureno kuingia nusu fainali. Goli lililowekwa wavuni na Cristiano Ronaldo lilitosha jana kuwafungisha virago Jamhuri ya Czech na kuyaaga mashindano haya. Ureno imekuwa timu ya kwanza kuingia katika nusu fainali ya mashindano haya. Leo jioni kutakuwa na patashika nyingine, wakati Ujerumani itakapominyana na Ugiriki, ambayo ina nia ya kuonyesha kuwa matatizo ya kiuchumi yaliyoko nchini humo hayaingiliana na soka. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ambaye ni shabiki mkubwa wa timu ya taifa ya Ujerumani anatarajiwa kuhudhuria pambano hilo jioni ya leo. Merkel hakuhudhuria mapambano ya timu hiyo katika awamu ya makundi yaliyofanyika nchini Ukraine.