Muigizaji maarufu wa nchini Marekani, Halle Berry, maarufu kwa sinema yake ya Catwoman, loosing Isaiah na When their eyes were wtching God, ameamrishwa na koti nchini humo kumlipa aliyekua mume wake, Gabriel Aubry, dola 20,000 kila mwezi sawa sawa na zaidi ya milioni 30 ya kitanzania, kwa kumsaidia kujikimu kwa mwezi na vile vile kumsaidia kumjali mtot wao pindi anapokua naye.
Halle Berry amepinga uamuzi wa jaji huyo na kukata rufaa ya kutaka kuhama nchini marekani na mtoto wake kuenda kuishi Ufaransa ambapo sheria za mapaparazzi na usumbufu ni zenye ukali zaidi kuliko zilivyo Marekani.
Staa huyo siye wa kwanza kumlipa mume pesa kwa mwezi kwa ajili ya kujikimu, kwani hata Britney Spears yalimkuta pale ambapo alilazimika kumlipa ex mume wake kiasi hicho hicho cha fedha kujikimu.
Kuoa Staa sometime bonge ya dili!!