OMOTOLA JALADE


Muziki, filamu ,fashion show kupamba Giraffe.
Nyota wa Filamu wa Nigeria, Omotola Jalade, anatarajiwa kutua nchini leo akitokea Nigeria ambapo usiku pia atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu iitwayo Super Star.
Omotola ambaye ataambatana na Meneja na mpiga picha wake maalum anatarajia kutua nchini leo kwa ndege ya shirika la ndege la Ethiopia. Omotola ambaye pia ni mwanamuziki, ni mmoja kati ya wasanii wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha katika soko la filamu nchini Nigeria. Kwenye orodha hiyo wapo poa Genevive Nnanji, Inni Edo na Ritha Dominick
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mwenyeji wa msanii huyo, Wema Sepetu alisema kuja kwa Omotola ni kufungua njia kwake katika soko la kimataifa la medani ya sanaa kwani lengo lake kubwa sasa ni kusonga mbele.
“Mikakati yangu ni kuingia soko la kimataifa nah ii ni njia ya kwanza ya kufanya hivyo, yapo mambo ambayo tutazungumza na kuangalia jinsi ya kufanya, suala si kuzindua SuperStar tu lakini pia kuona kiwango chetu,” alisema.
Katika onyesho la Giraffe, kiingilio kitakuwa sh 30000 kwa watu wazima ambapo watoto watalipiwa sh 5000 huku wakishuhudia filamu hiyo ya superstar, muziki utakaoporomoshwa na THT BAND, Onyesho la mavazi pamoja na nafasi kupiga picha na nyota huyo wa Nigeria.
Omotola ni mama wa watoto wanne ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16. Mumewe ni rubani na ndoa yao ilifungwa kwenye ndege ikiwa angani. Omotola alikuwa nchini Uingereza wiki iliyopita kwenye ziara za kikazi ambapo anakuja kwa uzinduzi wa SuperStar na kuelekea Marekani ambako kuna filamu anaenda kutengeneza.
Taasisi yake imeingizwa kwenye kinyang’anyiro cha kushindania tuzo bora ya kusaidia jamii. Hadi sasa nyota huyo amecheza jumla ya filamu 52, zikiwemo, Ties That Bind (2011), A Private Storm Ije (2010), My Last Ambition (2009), Beyonce & Rihanna (2008), Temple of Justice (2008), Tomorrow Must Wait (2008) na nyingine nyingi.