Well, si rahisi kufahamu mambo yake mengi sababu Miss Tanzania 2007, Richa Adhia amefanikiwa kuishi ‘a very low profile life’ kwa muda mrefu.
Mrembo huyo ni miongoni mwa mamiss Tanzania wa zamani waliojitenga na scandal kama maji na mafuta.
So story ni kwamba kuna jamaa mwenye bahati nyuma yake ambaye apparently ameshamtwanga lile swali muhimu, ‘will you marry me’!!
So who is the lucky guy? Ni mpenzi wake wa muda mrefu, Hridhaan Dhllon ambaye tayari ameshapiga magoti, akashika mkono laini wa Richa, akamtamza usoni kwa mahaba mazito huku akitamka, “will you marry me?”
That being said, Richa is this close to be officially off the market.
Kilichobakia sasa ni kwamba wapenzi hao kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuumaliza kabisa mchezo kwa kufunga ndoa iliwaanza maisha rasmi kama mume na mke.
Akiongea na G5CLICK mapema mwaka huu, Richa alisema, “Ni muda mrefu nimetangazia watu kuwa naolewa baada ya kuchumbiwa lakini kiukweli bado tunaweka mambo sawa, kikubwa tuombe uzima.
“Ila naomba watu waelewe kuwa ndoa za Tanzania si ngumu tofauti na za desturi ya kwetu kwani za Tanzania nyingi zinategemea michango ya watu ila za kwetu hakuna kuchangiana kivile hivyo yanahitajika maandalizi ya muda mrefu,” alisema Richa.