Kimora akiwa anafunga mume wake Djimon Hounsou ambaye ni staa Wa Blood Diamond aliyo cheza na Leonard Dicaprico


Hivi karibuni mwanamitindo na mjasiriamali Kimora Lee Simmons amekuwa kwenye vichwa vya habari nyingi kufuatia kuvunjika kwa ndoa yake na muigizaji Djimon Honsou. Pamoja na matatizo hayo ya ndoa, Kimora hajawahi kuacha kazi zake zinasimama. Kuna taarifa kuwa mrembo huyo anatarajia kwenda nchini Kenya.

Kimora anasemekana atakuwa mgeni rasmi katika tukio la mwaka huu la Fashion and Beauty (FAB) nchini Kenya.
Kwa mujibu wa gazeti la The Stars la Kenya, Kimora amekuwa akifanya mazungumzo na waandaaji japokuwa bado hajathibitisha kama atakuwepo kwenye tukio hilo la July ama December. “Kimora ana hamu kubwa ya kuitembelea Kenya na amekuwa akitweet kuwasiliana na miongoni mwa waandaaji,” chanzo kimoja kimeliambia gazeti hilo.

Tukio hilo la mwezi ujao linatarajiwa kufanyika tarehe 6-8. Kimora amewahi kuonekana kwenye filamu na vipindi vya televisheni kadhaa ikiwa pamoja na Beauty Shop, Brown Sugar, na Waist Deep. Ameshawahi kuonekana kwenye video za muziki za wasanii wa Marekani akiwemo Ginuwine na Usher, pia akiwa na reality TV show yake iitwayo Kimora: Life in the Fab Lane, inayooneshwa kupitia Style Network.