Pichani juu ni ajali ya ndege iliyotokea Jumatano Juni 20, 2012 katika jimbo la Katanga nchini DRC Congo. Ndege hiyo ilikuwa imebeba wafanyakazi wa migodi ya Mpweto na Dikulushi. Abiria wote waliokuwemo katika ndege hiyo walinusurika ambapo abiria mmoja alijeruhiwa kutokana na kutofunga mkanda.
Picha na Mdau Gervas ambaye ni mmoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika migodi ya Mpweto na Dikulushi.