Bondia Francis Miyeyusho (kushoto) akimshambulia bondia kutoka Malawi, John Masamba (kulia) wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi. Miyeyusho alishinda kwa KO raundi ya 5.


Bondia John Masamba (kushoto) kutoka Malawi akionyeshana ufundi wa kutupa masumbwi na Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.

Bondia Francis Miyeyusho (wa nne kushoto) akiwa ametulia wakati wimbo wa taifa ukiimbwa kabla ya pambano lake na Bondia John Masamba kutoka Malawi kuanza.