Mr Facebook usiku wa kuamkia leo amedondosha bonge la show jijini Nairobi Kenya katika show iliyokuwa imepewa jina la FAHRENHEIT PARTY.

Akiwa na madancer wake The Teddy Bears na Dj Soul T aliwafanya mashabiki wake kuutumia vema usiku wa kuamkia leo kwa show kali iliyokuwa na nyomi la kufa mtu

“That was a night well spent ‪#FAHRENHEITPARTY‬ – Big up @djcleo1,” aliandika shabiki mmoja.
Ilibidi ajifunze Kiswahili cha kuombea maji ambapo muda mfupi baada ya show alitweet, “ NAIROBI…. nataka msichana mrembo niyende naye south africa Akowaphi????? Hands up.” Japokuwa hatuna uhakika kama maneno haya aliyasema kwenye stage wakati akiendelea na show.

Dj Cleo alisindikizwa na wasanii kutoka Kenya ambao ni pamoja na kundi la Camp Mulla, Just A Band na Madtraxx.
Kuna kitu kimoja tu ambacho Dj Cleo kilimsikitisha jijini Nairobi kama alivyotweet kabla ya show, “FACT: Kenya has a shortage of ice, haven’t been able to get a drink with ice, I hope there’s some tonight when I get on stage LOL.”