Dr Edward Hosea

Baada ya kuwa kimya kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Dr Edward Hosea ameamka na kuamplfy jinsi walivyojipanga kukabiliana na vitendo vya rushwa sio tu kwa wanasiasa na viongozi wa serikali bali time hii wanaingia mpaka kwenye sekta binafsi ambako kunadaiwa ishu za rushwa zinafanywa sana hasa na wafanyabiashara.

Amesema “tungependa kila mfanyabiashara asaini makubaliano ambayo wamekubaliana katika sekta binafsi watakua nayo ambapo watu wote wanaofanya biashara watajizuia kuhonga kwa sababu kuhonga ni kinyume cha maadili ya kufanya biashara, najua nikisema hivi naweza kuonekana kama naota ndoto lakini bila kuweka taratibu za uadilifu katika sekta binafsi hongo itaendelea kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, ndio tumeanza na wao sekta binafsi katika mkakati wa kitaifa dhidi ya rushwa”