Producer na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya B’Hits Music Group Limited, Hermes Tarimo aka Hermy B amesema kama wasanii nchini wakiunganisha nguvu pamoja na kupigania haki zao ni rahisi kufanikiwa.
Kupitia mtandao wa Facebook jana Hermy B amesema umoja ndio njia pekee itakayowasaidia wasanii hao kupigana na kupata wanachostahili. “Natamani kuishi na kuona wasanii wote Tanzania wanafanikiwa, namaanisha kila mtu anayevuja jasho kwa ajili ya tasnia hii anastahili tuzo kwa namna fulani na nahisi kufanikiwa ni sehemu ya hili,” aliandika.

“Inaniuma sana ninapoona baadhi yetu tunafanikiwa na wengine hawafanikiwi, naumia napoona vipaji halisi vikipuuziwa na kutopongezwa, naumia sana ninapoona watu walionyuma ya utengenezaji wa nyota halisi wakipuuziwa na pengine walikilipwa kiduchu na mambo mengine yakikuzwa bila sababu.”

“Lakini moyoni mwangi najua; katika kila vita baadhi watafika mwisho na wengine hawatafika. Umoja ni kitu pekee kitakachotusaidia sisi kushinda vita vyetu vingi, hivyo natamani wasanii wa Tanzania waunganishe nguvu pamoja na kupigania haki zao, kupigania kile tunachostahili na kwakweli kupigana kwaajili ya mafanikio.”

source:bongo5