Miriam Odemba na Wema Sepetu


Meneja wa Wema Sepetu Martin Kadinda amesema kiwango cha pesa kilichotumika kumleta Omotola Tanzania sio chini ya dola elfu saba za kimarekani zaidi ya milioni kumi za kitanzania.

Amesema “mwanzoni tulikua tunataka kumleta Genevieve Nnaj lakini alikua busy na ratiba, tukamtafuta Ritha Dominic lakini gharama zake zilikua juu alikua anataka dola elfu 23 za kimarekani, nikaona itakua ngumu kwetu kwa sababu tunafanya wenyewe bila kuwa na udhamini baada ya kuhangaika ndio tukampata Omotola.

Omotola atakuepo leo pale Girrafe Ocean View kwa ajili ya family day, toka jana alitakiwa kuwa kwenye uzinduzi wa movie lakini kutokana na kupata matatizo kwenye ubalozi wa Tanzania Nigeria alichelewa ndege na kuingia Tanzania usiku sana.