Baada ya siku 49 za maisha ndani ya jumba la Big Brother, hatimaye mwanadada Barbz ameyaaga mashindano hayo.
Africa yenyewe ndio iliyoamua kumuondoa mwanamitindo huyo wa Afrika Kusini. Baada ya kutolewa kwa Barbz, Goldie wa Nigeria alisimama na kuanza kulia kwa uchungu mbele ya washiriki wengine na kuujutia uamuzi wake wa kumuokoa Prezzo na kumwacha rafiki yake kipenzi Barbz.

Mwanamuziki huyo wa Nigeria aliwaambia washiriki wenzake kuwa hakuwa anafikiria sawa pale alipomwokoa Prezzo badala ya Barbz.
Kwa upole, Barbz alimwambia Goldie “It’s okay.” Goldie alipiga magoti kuomba msamaha huku kila mmoja akionekana kupigwa na butwaa.

Barbz alipoambiwa kuwa muda wake wa kuendelea kuvuta hewa ya jumba la BBA umeisha, alimkumbatia kila mmoja na kwenda kwa Goldie kumpa ‘kumbatio’ la mwisho. Baadaye alikwenda kwenye Live Stage kwa mara ya mwisho na kumwambia mtangazaji wa Live Show, IK, kuwa amepata pigo la maisha kutokana na usaliti wa Goldie, “Bahati nzuri ni kuwa ninao watu wanaonipenda na watanijali nikirudi nyumbani,” alisema.

Katika hatua nyingine baada ya kujifanya na kiburi kwa siku kadhaa, hatimaye Prezzo amefungua mdomo wake na kumshukuru Goldie kwa kumwokoa dhidi ya eviction. Baada ya wakazi wa Upville kuwa kimya kufuatia kuondolewa kwa Barbz, Prezzo alimfuata Goldie juu nakumshukuru kwa kumwokoa na hatari ya kuyaaga mashindano hayo. “Thank you for saving my warrior a**. Nashukuru kwa kile ulichofanya,” alisema.

Goldie alionekana kuendelea kujuta kwa kumchagua Prezzo badala ya rafiki shoga yake Barbz. “Ningefanya nini kingine,” alimuuliza Prezzo bila kuhitaji jibu.

Kuondoka kwa Barbz kwenye BBA, kunazidi kuongeza nafasi ya Prezzo kuwa mshindi wa shindano hilo mwaka huu. Na sio sisi tu tunaohisi Prezzo anaweza kurudi Nairobi na kitita cha $300,000, hata MwanaFA anafikiria hivyo pia:

source:bongo5