Lupita uigizaji nyota wa shuga inayonyeshwa na MTV,

Kama umewahi kuiona series ya Shuga inayotengenezwa na MTV bila shaka ulishaiona sura ya mwanadada huyu mrembo mwenye ngozi nyeusi na nga’aavu kama bati lililoakisi mwanga wa jua, Lupita Nyo’ngo ana kila sifa ya kuwakilisha uzuri wa msichana asili wa kiafrikaa.

Baada ya kufanya vizuri kwenye show hii ya ‘Shuga‘, mrembo huyo amekula shavu la kushiriki kwenye movie ya Steve McQueen iitwayo ‘12 Years A Slave‘.

Kwenye movie hiyo atakutana na waigizaji ‘heavy weight’ wa Hollywood akiwemo Brad Pitt, Alfre Woodard, Chiwetel Ejiofor, Michael Fassbender, Ruth Negga, Adepero Oduye, Paul Dano, Benedict Cumberbatch, Scoot McNairy, Garret Dillahunt, Paul Giamatti na Sarah Paulson.

Kwa mujibu wa mtandao wa Hollywood Reporter, Lupita Nyo’ngo ataigiza kama mtumwa aitwaye ‘Patsey ambaye atajikuta akiteswa na kupendwa pia.
Filamu hiyo imetokana na kitabu kuhusu mtu mweusi,Solomon Northup, ambaye mapema miaka ya 1800s alitekwa na kuuzwa kama mtumwa na kukaa utumwani kwa miaka 12 kabla hajawa huru tena.

Chiwetel Ejiofor ataigiza kama Solomon Northup wakati Michael Fassbender ataigiza kama Mr. Epps.
hizi ni picha za watakao kuwa kwenye Movie hiyo

Brad Pitt

Ruth Nnega

Michael fassbender

chiwetel ejiofor

Alfre Woodard

Lupita akaiwa na waigizaji wezake wa shuga

Lupita

source:bongo5