Bingu Wa Mutharika


Chama tawala cha zamani cha nchini Malawi, DPP, kinashinikiza ufanyike uchunguzi dhidi ya mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua kutokana na kifo cha rafiki yake rais wa zamani wa Malawi, Bingu wa Mutharika.

TB Joshua


Katika ripoti iliyoandikwa kwenye gazeti la Nyasa Times, rais Joyce Banda alitangaza kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na kifo chenye mzozo cha kiongozi huyo wa zamani April 5, yakiwemo matibabu aliyoyapata.
TB Joshua alitabiri kifo cha Mutharika huku rais huyo mpya wa Malawi akiwa pia mtu wa karibu wa ‘nabii’ huyo kama ajiitavyo.
Msemaji wa chama cha DPP Nicholas Dausi, amesisitiza kuwa TB Joshua anatakiwa aulizwe maswali. Kifo cha ghafla cha Mutharika April 5 kilitokea miezi miwili kabla ya tarehe hii ambapo TB Joshua alisema rais wa Afrika atakufa baada ama ndani ya miezi miwili.

“Lazima tujue ni jinsi gani huwa anatabiri mambo” Dausi ambaye ni mbunge wa Mwanza Central aliliambia bunge la Malawi.
Dausi alitoa wito wakati akichangia bajeti ya nchi hiyo kuwa wananchi wa Malawi wapuuzie tambo za baadhi ya TV kama Emmanuel TV na TB Joshua kuwa walijua kutatokea kifo cha Mutharika.

source:bongo5