VITENDO vya kutupwa watoto wachanga vimezidi kushamiri ambapo leo asubuhi mwili wa kichanga kingine chenye jinsia ya kiume umeokotwa jirani na Msikiti wa Soweto jijini Mbeya. Mama wa mtoto huyo bado hajafahamika mpaka sasa. Tukio hili lanatokea ikiwa ni siku moja kuripotiwa tukio lingine la kuokotwa mwili wa kichanga mkoani Morogoro.

Mwili wa mtoto mchanga ukiwa umetupwa eneo la Msikiti wa Soweto jijini Mbeya leo asubuhi.

Baadhi ya wananchi wa eneo la Soweto waliofika kushuhudia tukio hilo.

Mwanausalama akiondoa mwili wa kichanga hicho eneo la tukio.

Akiupakia mwili huo katika gari la polisi.

SOURCE:kingkif