FAMILIA ya msanii wa filamu za Swahiliwood, Steven Kanumba, imeamua kuuza bidhaa za marehemu katika uwanja wa maonyesho wa Sabasaba uliopo Temeke katika kujenga utaratibu wa kumbukumbu dhidi yake.

Bidhaa za marehemu Kanumba kama aina ya nguo alizokuwa akipenda kuvaa, filamu alizowahi kuigiza, picha zake zitaonyeshwa katika maonyesho ya Sabasaba mwaka huu, familia ya marehemu imechukua banda kwa ajili ya maonyesho hayo ambayo yatakuwa ya aina yake kufanyika katika uwanja huo, anasema Magulu.

Katika banda hilo pamoja na kuona bidhaa za msanii huyo lakini pia kwa wale watakaolitembelea, watapata fursa ya kuongea na wanafamilia kama Seth Bosco mdogo wa marehemu aliyekuwa naye karibu sana, Mama yake mzazi, wafanyakazi wa kampuni yake.

Alisema hiyo itakuwa fursa nzuri kwa watakaotaka kujua mengi yamhusuyo Kanumba.

Kanumba alifariki miezi miwili iliyopita katika kifo kilichojaa utata huku msanii mwingine, Elizabeth Michale ‘Lulu’ akikabiliwa na kesi inayomtuhumu kuhusika na kifo hicho kilichotokea mara baada ya wawili hao kuzozana chumbani kwa Kanumba.