Raia wawili wa Iran wamefikishwa mahakamani mjini Nairobi nchini Kenya kwa tuhuma za kumiliki vifaa vya kulipuka kinyume cha sheria, ikiwa ni siku moja baada ya shambulizi la bomu la mkono katika baa moja lililosababisha vifo vya watu watatu mjini Mombasa.
Polisi nchini Kenya imewataja Wairan hao kuwa ni Ahmed Mohamud na Said Mausud, na kuwa walikamatwa wiki iliyopita kwa kuwa na mahusiano na kundi la kigaidi linalopanga mashambulizi ya mabomu mjini Mombasa na Nairobi.
Aidha Polisi wamesema vifaa vya kulipuka vilipatikana katika mji wa Mombasa kufuatia taarifa zilizotolewa na Wairan hao.
Mahakama ya jijini Nairobi inatarajiwa kupitisha uamuzi juu ya ombi la Wairan hao kutaka waachiwe huru kwa dhamana.
Waongoza mashitaka wameitaka mahakama hiyo kukataa ombi hilo.


source:dewjiblog