Wakiimba kwa mara ya mwisho mbele ya mashabiki 83,000 kwenye onyesho lililofanyika viwanja vya Dublin siku ya jumamosi, vijana waimbaji wa Westlife walopata mafanikio sana miaka ya 90 hadi 2000.
Akizungumza kabla ya onyesho Meneja wao Louis Walsh alisema ni kipindi cha maskitiko sana kwake, huku akidai hajawai kujua band kama hii na walikuwa na kipindi kizuri muda chote walichofanya kazi wote.
Kabla ya kufanya onesho hilo jumamosi Westlife walifanya tour mwezi Octoba 2011, kwa lengo la kuaga mashabiki wao.
Westlife wanatengana wakiwa na mafanikio makubwa katika tasnia ya muziki , wamewahi kushika No.1 mara 14 na wameuza nakara million 44 za album.