Masombo Lino kulia baada ya kumpokonya mpira Kiggi kama alimuazima, akitaka kugeuka kusukuma mashambulizi, Uwanja wa TCC jana.

BEKI wa Simba SC, Masombo Lino Masombo Lino kutoka Daring Club Motema Pembe kutoka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana alikuwa kivutio kikubwa katika mazoezi ya klabu hiyo Uwanja wa TCC Chang’ombe Dar es Salaam.
Kwenye mazoezi yaliyoongozwa na Kocha Mkuu wa klabu hiyo Mserbia Milovan Cirkovick, Masombo alionyesha ni mzuri kwenye kuzuia na kusaidia mashambulizi pia.
Mashabiki wa Simba walikuwa wenye furaha kubwa TCC jana kutokana na mavituuz yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wao wengine wapya pia.
Mazoezi ya Simba yanaendelea leo kwenye Uwanja huo kujiandaa na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame July 2013.
Beki huyu wa kati ambae alipiga soka la uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ametua bongo jana na leo imeelezwa limesaini mkataba, Simba mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara wamemsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani Yanga. (stori kutoka bongostaz.blogspot.zom)