Rihanna akiwa ndani ya gari baada ya kunusurika

Kikosi cha zima moto jijini London, Uingereza, kimesema mwanadada Rihanna ni miongoni mwa watu 300 waliotolewa kwenye moto ulioubuka mapema asubuhi jana kwenye lift ya hoteli hiyo.
Mwanamuziki huyo mwenye miaka 24, alitweet habari hiyo kwa wafuasi wake milioni 21 kwa kuweka picha ya gari la zimamoto na maneno yasemayo: “Roamin da streets since 6am! Fyah in da telly.”
Kikosi hicho kilisema king’ora cha hatari kililia saa 6:22 a.m. na askari kumi wa zimamoto walifanya kazi ya kuuzima moto huo uliozuka kwenye ghorofa ya saba ya hoteli ya kifahari ya Corinthia. Hakuna ripoti za majeruhi kutokana na moto huo.
Rihanna yupo nchini Uingereza kwa zaidi ya wiki moja sasa ambako amekuwa akifanya show mbalimbali ikiwa pamoja na kuwapa support Jay-Z na Kanye West ambao wapo ziarani barani Ulaya iitwayo ‘Watch the Throne Tour’.
Rihanna, Jay-Z, David Guetta na Elton John watakuwa miongoni mwa watumbuizaji kwenye sherehe ndefu za “London 2012 Festival’, ambazo zimeandaliwa kote nchini Uingereza kwendana na michezo ya kiangazi ya olimpiki mwaka huu mjini London.
Sherehe hizo ambazo zimeanza, zitaendelea hadi Sept. 9, na kujumuisha matukio na performance 12,000.
Kutakuwepo na matukio mbalimbali katika masuala ya filamu, muziki, mitindo, sanaa za majukwaa, dance na sanaa za mikono.
Website ya mtandao huo imesema hizo ni sherehe kubwa kuwahi kufanyika nchini Uingereza zikiwa na bajeti ya takriban dola milioni 86.