Yvonne Nelson on Cover Page

Muigizaji mwenye scandal kibao lakini mwenye kipaji cha hali ya juu nchini Ghana, Yvonne Nelson ameibuka kuwa muigizaji anayelipwa mkwanja mrefu zaidi nchini humo na kuwashinda wengine kama Jackie Appiah na Nadia Buari.
Waigizaji hao watatu kwa mujibu wa utafiti walikuwa ‘madiva’ wanaotafutwa zaidi huko Ghollywood na sasa Yvonne ambaye amekuwa akihusika na scandal kibao amekamata nafasi ya kwanza katika list hiyo.
Yvonne, model, designer,mfanyabiashara na muigizaji aliyeshirikishwa kwenye filamu lukuki za kimataifa huku mpya akiwa ameigiza kama Halima Abubakar kwenye ‘Mistress’ hafanyi mazungumzo kwa ‘madafu’ ya Nigeria (naira) bali ni kwa dola ya Marekani tu.
Na sasa bila dola 10,000 mezani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 15 za Tanzania hawezi kufanya movie.
Bei yake hiyo kubwa tayari imewafanya baadhi ya waandaji wenye bajeti ndogo kusitisha mipango yao ya kumtumia kwenye filamu zao.
Pamoja na kumlipa $10,000, kuna masharti na vigezo vingine vinapaswa kuzingatiwa na kama asipoviona, bado producer anaweza kuondoka na hela zake.
Kwa sasa mrembo huyo amelamba mkataba mnono wa matangazo na kampuni ya Vodafone

source:.bongo5