Asasi ya EDUCATE THE CHILDREN ni asasi ya kijamii iliyoanza mwakak 1998 ikiwa na lengo la kuchochea upatikanaji wa elimu bora na kwa namna ya pekee kwa watoto wa familia duni. Asasi hii inaendesha shule ya msingi na awali ya St. joseph’s iliyoko Mbezi Beach, Dar es Salaam. Shule hii inasifika wa viwango vizuri vya ufaulu tangu kuanzishwa kwake.
EDUCATE THE CHILDREN imepanga kufanya uzinduzi rasmi wa mfuko wake wa elimu ikiwa na lengo la kutunisha mfuko utakaosaidia watoto wa familia duni katika shule ya St. Joseph’s. Tangu kuanzishwa kwake shule imekuwa na utaratibu wa kusaidia baadhi ya wanafunzi ambao wameshindwa kuhimili gharama za masomo kutokana na kupatwa na majanga mbalimbali katika familia zao. Kutokana na kuongezeka kwa gharama za kuendesha shule na kuongezeka kwa uhitaji, imeonekana ni busara kutenganisha mfuko huu na gharama za kila siku za shule na vile vile kualika wadau wengine wenye nia njema na matamanio ya kuendeleza elimu Tanzania.
Harambee ya uzinduzi wa mfuko huu itaongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dr. Alex Geaz Malasusa. Kutakuwa na chakula cha hisani ili kuwezesha zoezi hili litakaloanza saa saba na nusu mchana Jumamosi tarehe 30 Juni.
Tunapenda kuwakarinbisha watanzania wote wenye nia njema kutuunga mkono kwenye jambo hili jema kabisa. Tunawakaribisha kwa namna ya pekee wale wenye majina ya Joseph kushiriki nasi, tutakuwa tumeandaa meza maalumu kwa wote wenye majina ya Joseph siku hiyo ili kumuenzi somo wa shule yetu.
Tunawakaribisha vile vile mablogger kushiriki nasi. Tumeandaa nafasi maalumu kwa ajili yenu na mnaweza kushiriki kuhabarisha watanzania kuhusu tukio hili siku yenyewe ya tukio. Tunawaomba vile vile mshirikishe na wadau wengine kupitia mitandao ya kijamii na blogu zenu ili kuweza kujenga mwamko wa suala hili jema.
Tunapenda kuwashukuru sana wadau mbali mabli; mashirikika, wafanyabiashara na watu binafsi waliojitolea kutuunga mkono mpaka dakika hii. Tunawashukuru kwa namna ya pekee Clouds Media Group kwa kuwa nasi bega kwa bega katika shughuli hii.
Tunaamini mashujaa hawazaliwi, wanatengenezwa. Nasi tumetoa nafasi ya kutengeneza mashujaa hawa.

KARIBUNI SANA!!!
Wenu katika maendeleo ya elimu,
Deus Valentine,
Katibu Mtendaji – EDUCATE THE CHILDREN.

source:dewjiblog