Akiwa tayari amesign mkataba wa kuichezea Simba SC msimu huu, mchezaji kiungo Mussa Mudde (Pichani) kutoka timu ya taifa ya Uganda anatarajiwa kuwasili jijini Dar-es-salaam leo kwaajili ya kukamilisha taratibu mbalimbali za uhamisho.
Mzungumzaji wa Simba SC Ezekiel Kamwaga amesema tayari Mudde amesajiriwa kwa mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo ya Msimbazi.
Mudde ambaye ameichezea timu ya Sofapaka kutoka Kenya kwa kipindi cha miaka miwili na nusu, sasa anajiunga na Mganda mwenzie Emmanuel Okwi kuitumikia Simba SC.