Hali ya afya ya Dkt. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania, inaendelea vyema baada ya kushambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam.
Dkt. Ulimboka aliokotwa jana akiwa hajiwezi na mwili ukiwa na majeraha mengi baada ya kupigwa na watu hao na baade kufikishwa Hospitali ya taifa Muhimbili na wasamaria wema.
Ulimboka anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhumbili kitengo cha mifupa MOI aliko lazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku jopo la madaktari Bingwa wakiendelea kumnusuru.

source:fatherkidevu