MREMBO Lisa Jensen anaeshikilia taji la Redd’s Miss World Tanzania, na ambaye ataiwakilisha nchi katika mashindano ya mwaka huu nchini China amewasili jana mkoani Mara tayari kushuhudia shindano la Miss Mara 2012 litakalo fanyika kesho Ijumaa juni 29, katika ukumbi wa Musoma Club. Pichani ni Lisa akiwa na Mratibu wa shindano hilo, Godsos Mkama na Mwalimu wa wanyange wa Mara Loveness Flavian Mrembo mwenye taji la Sports Woman Miss Tanzania 2011.

Washiriki wa shindano la Redds Miss Mara 2012 wakiwa katika picha ya pamoja katika ufukwe wa Ziwa Victoria, mkoani Mara baada ya mazoezi yao jana. Warembo hao wanataraji kupanda jukwaani Ijumaa, Juni 29, 2012 kuchuana vikali kuwania taji la mkoa wa mara na tiketiketi ya Kushiriki shindano la Redds Kanda ya Ziwa.


Jumla ya warembo tisa wanataraji kupanda jukwaani Ijumaa hii katika ukumbi wa Musoma Club kuwania taji la Redds Miss Mara 2012.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, Mwandaaji wa shindano hilo, Godson Mkama wa Entertainment & Promotion, amesema warembo wote wapo shwari na wanaendelea na mazoezi yao chini ya mwalimu Loveness Flavian Mrembo mwenye taji la Sports Woman, upande wa Dance wanafundishwa na Bokilo toka T.O.T.
Amesema Burudani itakayo sindikiza ni kutoka kwa Wasanii Wakali toka Jijini Dar es Salaam ambao ni Professor J, Sharo Millionea na Wasanii wa kutoka Kanda ya Ziwa.
Amewataja walimbwende hao wanao wania taji hilo kuwa ni pamoja na Jacqueline Mzava, Lona Kisalila, Justine Thomas, Veronica Jackson, Namsi Mnubi, Rose James, Eugenia Fabiano, Jesca Sprian na Aisha Bakari
Wadhamini wa shindano hilo ni African Barrick Gold, Redds Orginal, Crdb Bank Limited,Coca Cola, Mara Security Guard, Hotel Maltivilla, Musoma Club, Musoma Utalii Collage, Mapa Traders na Msendo Mini Supermarket.

source:Fatherkidevu