Wakati msimu wa mwaka 2012 wa ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani, NBA umemalizika wiki hii kwa timu ya Miami Heat kuchukua ubingwa, baadhi ya wachezaji wameanza kuhamia timu mpya.
Lamar Odom aliyekuwa akiichezea Los Angeles Lakers sasa anahamia kwenye timu nyingine ya jiji hilo hilo, L.A. Clippers.
Kubaki kwa Lamar jijini Los Angeles kumepokelwa kwa shangwe na mke wake Khloe Kardashian, ambaye atabaki kuwa karibu na familia yake jijini Los Angeles.
Jana, chanzo kimoja kimeliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Odom alikuwa na mazungumzo na Dallas Mavericks, Clippers, na Utah Jazz.
Kwa sasa imetangazwa rasmi kuwa ataichezea timu hiyo aliyoanza nayo mwaka 1999.
Akiendelea kuishi Los Angeles atakuwa na muda mzuri kuanzisha familia yao wenyewe na mkewe Khloe.
Mapema mwaka huu nyota huyo wa show ya Keeping Up With the Kardashians, alianza matibabu kwaajili ya kumwezesha kushika mimba kwenye kliniki ya L.A.