Kampuni ya usambazaji wa filamu za kitanzania Steps Entertainment ya Jijini Dar-Es-Salaam ikishirikiana na Msanii wa filamu wa Bongo Movies, Vincent Kigosi almaarufu kama Ray, wametoa Msaada wa vitu mbali mbali kwenye kituo cha watoto yatima cha Maunga Center kilichopo maeneo ya Kinondoni ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa filamu yake mpya.

Msaada huo ni sehemu ya mpango wa matukio ya uzinduzi wa filamu yake ‘Sobing Sound’ na pia kurudisha fadhila kwa jamii ambayo ndio wateja wakubwa wa filamu za kitanzania.

Filamu hiyo imezinduliwaa kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua ukumbini kama ilivyozoeleka na wasanii wengi, msanii huyo ameamua kuzindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5.

Akizungumza na http://www.bongo5.com mara baada ya kuzindua filamu hiyo, akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray, ambaye pia aliongozana na afisa masoko wa kampuni ya steps,bwana Ignatusu Kambarage ,alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutaabika, kitendo ambacho amesema, si kizuri.


Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri ,na atahakikisha japo kidogo,kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima, kwani anawapenda.

“Hii ni filamu ya kwanza kutoa, tangu kifo cha mwigizaji mwenzangu Steven Kanumba alipofariki dunia, Aprili mwaka huu, na najisikia furaha kuja hapa na kutoa msaada kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu” alisema Ray

source:bongo5