Hatimaye ndoa ya waigizaji wakubwa kabisa wa Hollywood Tom Cruise na Katie Holmes imefikia tamati.
Holmes alitangaza jana kupitia mwanasheria wake kuwa amewasilisha nyaraka za talaka dhidi ya mume wake Tom Cruise waliyedumu naye kwa miaka mitano.
Habari hizo zimeushangaza ulimwengu wa filamu unaomchukulia Cruise kama kati ya waigizaji wanaofahamika zaidi.
Cruise aligundua kuwa Holmes ameanzisha mchakato wa talaka jijini New York wakati yeye akiwa anaigiza filamu huko Iceland.
“Tom amehuzunishwa sana na anawaangalia zaidi watoto wake watatu. Tafadhali wapeni muda wao kuyakabili hayo,” alisema msemaji wake.
Mwakilishi wake wa siku nyingi Bert Fields amesema Tom bado hajamwajiri wakili wa masuala ya talaka.
Holmes, 33, ameajiri makampuni mawili maarufu yaliyojikita kushughulikia talaka zinazohusisha utajiri mkubwa.
Cruise ameshawahi kuwa na wake wawili wengine wa Hollywood, Mimi Rogers na Nicole Kidman.
Kipato chake kwa mwaka kwa mujibu wa Forbes ni dola milioni 75.