FFU ! Ngoma Africa Band Wamemaliza kazi Dortmund,Ujerumani,
Mzimu wa Dansi unazidi kupagawisha Ughaibuni

Dortmund,Ujerumani,
Wadau na wapenzi wa muziki katika maonyesho ya Afro-Ruhr Festival,siku ya jumamosi 30.06.2012
walijikuta wakizolewa na mdundo wa dansi wa bendi maarufu barani ulaya “Ngoma Africa band” aka
FFU, Kikosi kazi hiko kilifanikiwa tena kujiwekea rekodi ya pekee kwa kujizolea washabiki wanao ukubali
mdundo wa bendi hiyo,baadhi ya washabiki walishindwa kujiziwia ! kwa utamu wa muziki walihamua
kuvamia jukwaa.
Bendi maarufu inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja wa FFU,imejaa wanamuziki wenye bidii
akiwemo Soloist Afande Chri-B, Kikosi kazi cha Ngoma Africa kimezidi kujiimarisha kwa sasa ina
idadi ya wanamuziki 14 ,ambapo zamani ilikua na wanamuziki 8,wanamuziki wengi chipukizi wamejiunga
na Ngoma Africa band kwa nguvu moja ya kutaka kuimarisha na kuitangaza miziki ya Bongo na Afrika mashariki
pia,Ngoma Africa band inaonekena ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya yenye kuwa na washabiki na waufuasi
wengi wa mataifa,umri mbali mbali, bendi ambayo washabiki wanadai kuwa ni mali yao ! na Ras makunja na
wanamuziki ni watumishi wa washabiki tu.
Bendi hiyo maarufu kwa sasa wanatamba na CD mpya ya “Bongo Tambarare” ambayo ina nyimbo za
“Supu ya Mawe” na “Uhuru wa Habari” unaweza kuzisikiliza at http://www.ngoma-africa.com au
sourcengoma-africa.