Mwanamuziki wa kike nchini Tanzania aliyewahi kutamba na wimbo ‘Njia Panda’, Doreen Aurelian Cassian Ponera aka Pipi, ameamua kuweka wazi furaha aliyonayo kwa kuwa mama mtarajiwa.
Pipi ambaye kwa sasa ana wimbo mpya uitwao ‘Unapokuwa mbali’ ameyaondoa mashaka waliyokuwa nayo baadhi ya watu walioiona video hiyo na kugundua kuwa kuna mabadiliko kwenye saizi ya tumbo lake na hivyo kuhisi kuwa tayari ni mjamzito.
Jana kupitia Facebook ameamua kuonesha live tumbo lake na kuwapa jibu wale walioukuwa na mashaka na hali yake ya sasa.
Kitendo chake cha kuwa wazi kiasi hicho na kujivunia kuwa mama mtarajiwa, kimesifiwa na watu wengi.
“It’s hard kwa wanawake wengi kudisclose their affairs especially pregnancy but umeweza, unastahili pongezi kwa kweli, kwanza kwa kukubali kuitunza mpaka hapo maana wengi hupendelea abortion,” aliandika mmoja wa rafiki zake.
Nasi pia baada ya kuona picha hizo tulimtupa pongezi kwa ujasiri huo kwa kumwambia, “Naona you are a proud mama to be! Hongera sana,” na yeye akajibu, “Hahaha, yes am very proud, thanks a lot!

source:bongo5.