Balotelli akiwa na mama yake pamoja na mpenzi wake wa zamani

Pamoja na kutokwa machozi kama mtoto wa shule juzi kutokana na kipigo ‘kitakatifu’ cha Hispania dhidi ya Italia kwenye fainali za Euro 2012, walau mshambuliaji Mario Balotelli ana kitu cha kumfuta machozi.
Mpenzi wake wa zamani Raffaela Fico ni mjamzito wa mtoto wake.
Hivi karibuni Raffaella alionekana kwenye tukio la utoaji wa misaada mjini Rome akionekana wazi kuwa ni mjamzito, hali iliyopelekea watu wengi kuamiani kuwa mimba hiyo ina miezi kadhaa.
Model na nyota huyo wa television hivi karibuni alithibitisha habari zilizoandikwa na gazeti la Sport Mediaset, kwa kusema, “Nilimpigia simu kabla ya mechi yao dhidi ya Ujerumani na kumwambia, nategemea kupata mtoto, ni mtoto wako. Baada ya muda aliniambia, “Umenipa habari nzuri kuliko zote duniani.”
Ingawa mshambuliaji huyo wa Manchester City na Fico waliachana miezi miwili iliyopita, gazeti la Daily Mail liliripoti kuwa Fico alisema Super Mario anataka warudiane ili kumlea mtoto wao.

source:entertainment.myjoyonline.com