Mwanamuziki wa kizazi kipya cha lingala ya Congo, Fally Ipupa amezidi kuonesha ukaribu zaidi na wasanii wa Nigeria na kufanya nao ngoma.
Jana kupitia Facebook, alipost picha mbili akiwa kwenye ‘video shoot’ nchini Ufaransa na msanii wa Nigeria Flavour na kumaanisha kuwa wamefanya wimbo pamoja.
Wimbo huo mpya ni wa Flavour utakaokuwepo kwenye albam yake mpya.
Fally Ipupa amewahi pia kushirikishwa na Jay Martins katika remix ya wimbo wake uitwao Jukpa.
Jumamosi iliyopita, June 30, Flavour, kundi la Bracket na Dontom, walikuwa mjini Paris Ufaransa kwa mara yao ya kwanza na kutumbuiza mbele ye umati wa wapenzi wao wa muziki nchini humo.
Ziara hiyo ilimpa nafasi Flavour ya kumpata Fally Ipupa ambaye mara nyingi huwepo Paris na kufanya video yao jana.
Wasanii wa Afrika kutoka nchi zingine zisizozungumza kifaransa, wameanza kujipatia soko na umaarufu mkubwa nchini Ufaransa husasan wasanii wa Nigeria.
Mwezi March mwaka huu Flavour N’Abania alisaini mkataba na label kubwa ya muziki ya nchini Afrika Kusini iitwayo Sould Candi.
Mkataba huo ulifanikisha uuzwaji wa albam yake Uplifted, iliyokuwa na hit ‘Nwa Baby’ kuuzwa nchini Afrika Kusini.
Kwa upande wake Fally Ipupa, mwishoni mwa mwezi uliopita, aliungana na Ferre Gola mjini Paris kuimba wimbo wa kizalendo kwa nchi yao uitwao “Congo, my country.”
Wasanii wengine wa Congo walioshiriki kwenye wimbo huo ni Lokwa Kanza, Djessi Matador, Aimelia, Celeo Schramme na wengine ambapo jumla wapo wanamuziki 30.