Waandaji wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika kila mwaka mwezi February visiwani Zanzibar, wamesema wanajitahidi katika tamasha la mwakani, 2013, kuleta wasanii wakubwa wa nchini DRC.
Extra musica, JB Mpiana, Werrason na Fally Ipupa ni miongoni mwa wasanii ambao wangependa kuwaona kwenye steji wakati tamasha hilo la kumi litakapofanyika tarehe 14 hadi 17 February, 2013 mjini Zanzibar.
Ni wasanii wachache sana kutoka Congo waliowahi kutumbuiza katika tamasha hilo kubwa wakiwemo Fredy Massamba, Samba Mapangala na orchestra Virunga and Super Mazembe.
Waandaji wa tamasha hilo wamesema lengo lake ni kupromote vikundi vya muziki vya Tanzania kwa walau asilimia 50 na asilimia zingine ni kwaajili ya wasanii kutoka nchi zingine za barani Afrika pamoja na waafrika waashio ugenini (Diaspora).
Wamesema awamu ijayo wangependa kuwaalika wanamuziki wanaojulikana zaidi wakiwemo Extra Musica, Fally Fally, Werra Son, JB Mpiana, Staff Benda Bilili, Konono No. 1, Kasai All Stars na wengine.
Wamesema wanamuziki hao watakonga nyoyo za wapenzi wa muziki na pia kuwabadilisha wasanii wa Tanzania katika kutengeneza muelekeo mpya kwa kufanya muziki halisi wa kitanzania.
Tamasha hilo ambalo hufanyika kwenye eneo la ‘Ngome Kongwe’ mjini Zanzibar huwakutanisha wasanii wakubwa wa Afrika, wapenzi wa muziki na waandishi wa habari kusherehekea utajiri wa muziki wa bara la Afrika.

source:bongo5