Kiongozi wa G-Unit, 50 Cent aliamua kubadilisha mawazo yake kuhusu albam yake mpya ya Five (Murder By Numbers) kwa kuitoa bure wiki hii na kusema kuwa albam yake rasmi akiwa chini ya Interscope Records itatoka mwezi November mwaka huu.
“You can’t buy album 5 it’s FREE street king immortal will be for sale#SMSaudio” (50 Cent’s Twitter)
Albam hiyo imetoka rasmi jana na kuongeza kuwa, “My official Interscope album is called STREET KING IMMORTAL due out in nov”
Katika mahojiano na mtandao wa All Hip hop mwezi May mwaka huu, 50 alisema kuwa ataachia albam yake July 3, bila kujali kama itafanyiwa promotion ya kibiashara ama la.
Aliongeza kuwa aliamua kufanya hivyo kwendana na siku yake ya kuzaliwa ambayo ni jumamosi hii ya July 7.